Waumini walipata nafasi ya kujikumbusha ujumbe wa Arubaini - msisitizo wa upendo, kujitolea na mshikamano wa Kiislamu -sambamba na kushiriki kwa vitendo katika kuokoa maisha kupitia uchangiaji damu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waumini kutoka vituo vya Ngare Nairobi, Mwangaza na Matadi, wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wakiongozwa na Sheikh Said Shekigenda -Mkuu wa Kanda hizo- waliadhimisha kumbukumbu ya Arubaini ya Mashahidi wa Karbala mnamo tarehe 15 Agosti 2025.
Sehemu ya maadhimisho hayo ilihusisha kampeni ya uchangiaji damu katika Zahanati ya Ngare Nairobi, ikiwa ni sehemu ya kuenzi thamani ya kujitolea kwa Imam Hussein (a.s) na mashahidi wenzake.
Katika majlis hiyo, Sheikh Ma’amun Husein Adamu alikuwa mzungumzaji mkuu ambapo alitoa mada kuhusu “Fadhila za Kumtembelea (Kumzuru) Abā ‘Abdillāh al-Hussein (a.s)”.
Waumini walipata nafasi ya kujikumbusha ujumbe wa Arubaini – msisitizo wa upendo, kujitolea na mshikamano wa Kiislamu – sambamba na kushiriki kwa vitendo katika kuokoa maisha kupitia uchangiaji damu.
Your Comment